Nchi ya urithi
Auteur : Suleiman Ali Ali
Date de publication : 2017
Éditeur : Ali Suleiman Ali
Nombre de pages : 194
Résumé du livre
"Upepo uliukimbiza wena wa viongozi wa nchi. Roho zao zimejaa kutu isiyosafishika hata kwa msasa wenye neema za waumini. Waliyaskika mamlaka kw viapo mbele ya manani huku wakiahidi kuwatumikia wengine kwa haki. Nafsi za raia zikajenga bashira ndefu kwa walioshika mamlaka kwanba hiyo ndio neema yao. Maskini wanyonge hawa, sasa wananyanyasika na kuupoteza uhai. Zile tamaa na tumaini zilizowajaa nafsini mwao sasa zimegeuka damu itokayo nyamani mwao. Wanateswa na kuuawa bila sababu. Hakuna haki stahiki iliyosimama kwao. Nchi imekuwa ya urithi. Viongozi wanafaidi matunda na neema iliyowastahikia raia. Wanarithishana madaraka kwa lengo la kuyafaidisha matumbo yao. Guela anakaribia kuupoteza uhai wake mbele ya umma iliomkabidhi sadaka ya mioyo yao kwa ajili ya kuitafuta haki. Damu yake inamwagika baada ya kutumikia kifungo cha singizio na damizo."--Page 4 of cover